DiscoverSiha Njema
Siha Njema
Claim Ownership

Siha Njema

Author: RFI Kiswahili

Subscribed: 8Played: 64
Share

Description

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

186 Episodes
Reverse
Mwongozo wa  shirika la afya duniani,WHO kuhusu usafi,unapendekeza choo kimoja kinaweza kutumika na watu 20 ila katika kisiwa cha Ndeda ndani ya Ziwa Victoria ,watu zaidi ya elfu 2 wanachangia vyoo vitano
Kama kuna kipindi watu wengi huwa tumbo joto, ni kusubiri matokeo ya kipimo cha HIV au magonjwa mengi ya zinaa.Au kuambiwa huna uwezo wa kizazi. Hata hivyo unapofanya vipimo hivyo itakuokoa kufanya makosa ambayo yanaweza kuathiri familia yako baadaye. Ikiwa utapima baadhi ya vipimo hivi muhimu utaweza kujipanga kifedha na kuchagua matibabu ambayo yanaweza kutatua changamoto za afya ambazo pengine umekutwa nazo.
Watu wengi wanapokaribia kufunga ndoa,hujukumika kufanya vipimo vya virusi vya HIV .Wengi hufanya kipimo hicho si kwa sababu wanajua umuhimu wake bali ni kwa sababu ya ulazima kabla kufunga harusi haswa za Kikristo. Hata hivyo watalaam wa afya wanasema kuna vipimo tele ambavyo ni muhimu pia na vinahitajika kufanywa kabla ndoa. Mwanasaikolojia Naomi Ngugi  anasema kando na kipimo cha HIV,kuna  kipimo cha Rhesus Factor ambayo kama mtu na mwenzake hana ufahamu ,wanaweza kupata shida ya kuharibika mimba. Kuna pia kipimo cha  Genotype  kubaini uwepo wa ugonjwa kama  Selimundu ,Hepatitis B,  Hepatitis C au homa ya ini,vipimo vya  Magonjwa sugu, Magonjwa ya akili na Vipimo vya uzazi kubaini ubora wa mbegu za kiume na matatizo ya  mirija kuziba upande wa wanawake.   Vipimo hivyo vinaweza kugharimu ndoa iwapo wanandoa hawataweka wazi.
Vyakula vinavyoandaliwa nje ya jikoni kwangu huwezi kufahamu viwango gani vya usafi vimezingatiwa Unapoaumua unakula kwa mama nitilie ni vigezo gani unaweza ukaweka ili kuhakikisha unalinda afya yako? Alfred Lobawoi kwenye makala haya ,amewahoji wauza vyakula na walaji kujua mtazamo wao
Juhudi za serikali za Afrika kuja na mikakati ya kutoa huduma za afya kwa raia kupitia mipango ya bima ya afya ya kitaifa zimekabiliwa na changamoto za utekelezaji,ufisadi na mifumo isiyo thabiti. Watalaam wa afya sasa wanapendekeza mipango hiyo ya afya iwe kwenye mipango ya kitaifa ya kila mwaka,ikiwa na mwongozi kamili kuhusu huduma gani serikali itatoa kwa raia na kwa kiasi gani. Aidha watalaam wanashauri mipango hiyo iwe inaendana na mahitaji ya kila jamii kwa kuwa serikali nyingi kwa sasa hazina uwezo wa kutoa huduma zote kwa raia Isitoshe,mifumo inyopunguza uvujaji wa raslimali  za umma ni muhimu
Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo  hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe  na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi. Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au  kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka. Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.
Hivi karibuni watalaam wa afya pamoja  kwa ushirikiano na  shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini. Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi hudhani kuwa Pneumonia husababishwa na baridi kuingia kwenye kifua lakini watalaam wanasema chanzo cha Pneumonia ni vimelea kushambulia mapafu na mfumo wa kupumulia Watalaam wa afya wanasema ndani ya wiki moja, mtu aliye na Pneumonia hugundulika kwa kuwa anapata ugumu wa kupumua au hata kukosa hewa.
Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika  imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla. Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu. Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu  wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu. Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo kwa wakati mwingi huwekeza kwenye miradi inayozingatia matakwa yao. Aidha ili kuhakikisha kuwa huduma za afya kama uchomaji chanjo zinawafikia wanajamii wote ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kuimarisha huduma za wahudumu wa afya wa jamii ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawafikia watoto walengwa baadala ya wazazi kupata ugumu wa kwenda kusaka huduma hizo.
H pylori isipotibiwa inaweza kugeuka kuwa saratani ya tumbo ,watalaam wameonya Katika makala haya,tunaangazia  sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kupata maambukizo ya H pylori na matibabu yake. Matibabu yake kwa mujibu wa daktari Alex Mungala anayehudumu jijini Nairobi yanaweza kukabiliwa na usugu wa vimelea ,ni ghali na si rahisi kupatikana katika vituo vya afya vya daraja la kwanza.
Utafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na  kupoteza kumbu kumbu Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya. Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu. Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi  la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku. Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi. Wapo waliokuwa na wanatumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu na sasa wameachana nazo. Aidha wengine wameeleza matembezi kuwaondolea maumivu ya viungo na pia kupata marafiki wazuri.
Kukaa kwa zaidi ya saa sita mfululizi kila siku inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya uti wa mgongo,kisukari,shinikizo la damu na kifo cha mapema
Katika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema polisi wenye changamoto za afya ya akili hawatafukuzwa kazi bali watapewa matibabu stahiki Kumeshuhudiwa hivi karibuni visa vya polisi kutumia silaha zao visivyo na utendakazi wao kukosolewa na raia pamoja na wanaharakati wa haki
Hivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila  kushinikizwa .
Takwimu zinaonesha watu wengi kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kuishi bila kufanya mazoezi na kula vibaya Sera hii itatoa mwongozo wa  taasisi za serikali na binafsi kuweka mikakati ya kuruhusu mazoezi ya kila mara wakati wa kazi au nje ya kazi
Kila siku mwili wako hukuzungumzia na ni jukumu lako kusoma mwili wako na kuelewa unasema nini au unakuonya kuhusu nini Baadhi ya matatizo ambayo unaweza kujiepusha nayo ni matatizo ya afya ya akili ,kufeli viungo muhimu au mifumo yako ya afya. Na ili kuhakikisha mwili wako unazungumza na kutoa taarifa iliyo sahihi kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kwa mfano kupata muda wa kutosha kulala,kupata lishe bora  na kufanya mazoezi 
Matatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa  dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali  kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid  Disease Awareness Kenya Foundation ,TDAK,  Sarah Katulle anaelezea umuhimu wa wagonjwa kuwa kwenye kundi ambapo wanaweza kushirikishana kuhusu mbinu mbadala ya kuishi na matatizo hayo kando na matibabu. Kundi hilo linawasaidia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa ,mahabara maalum na dawa sahihi. Aidha TDAK ili kuwasaidia wagonjwa hao kuishi maisha ya kawaida wakiwa kazini ,inawaandikia barua ambazo zinawasilishwa kwa maajiri kutambua hali halisi ya wagonjwa na mahitaji yao.
Misri ipo kwenye njia panda  kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta  mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya  serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa  za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi  na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho la pili sheria zake za kutoza ushuru bidhaa za tumbaku iwapo lengo ni kuleta mapato kwa serikali ,kuwafaidi wazalishaji au kwa maslahi ya afya ya wengi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,WHO,  asilimia 20-25% ya watu wazima nchini Misri huvuta sigara.
Kabla mgonjwa yeyote kuanzishwa kwenye  matibabu, awe ana tatizo la tezi koo kuzalisha homoni kupitiliza au kushindwa kuzalisha, ni sharti vipimo maalum kufanyika Kipimo cha kwanzo ni inaangazia homoni tofauti inayozalishwa na tezi koo na hii mtu yeyote anaweza kufanya katika wakati wa kufanya vipimo kujua hali yake ya afya ,hapa mtu si lazima awe ameonesha dalili za tezi koo kuwa na tatizo.Kipimo cha pili ambacho ni muhimu huzingatia zaidi  viwango vya  homoni tatu muhimu zinazozalishwa na tezi koo ambayo ni  (TSH), thyroxine (T4), na  triiodothyronine (T3) .Matokeo yataamua ni mpango gani wa matibabu mgonjwa atapewa  dawa,kudhibiti homoni au kuzalisha homoni mbadala tezi koo inaposhindza kazi yake.Kando na dawa kama mpango wa matibabu ,wagonjwa wenye uvimbe wanaweza kushauriwa kufanya upasuaji kuondoa tezi koo ,sehemu yake au yote.Kuna pia mpango wa kutumia mianzi na madini ya Iodine maarufu kama Radioiodine mpango ambao ni sharti kufanywa kwa ueledi mkubwa na kwenye vituo vya afya vilivyo na vifaa vya viwango vya juu.
loading
Comments